• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika zashirikiana kutoa pendekezo la "kuhimiza na kulinda haki za binadamu kwenye maendeleo"

    (GMT+08:00) 2019-07-10 09:23:32

    Mkutano wa 41 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa umefanyika hivi karibuni ambapo wajumbe wa kudumu wa China na wa nchi za Afrika walikutana kando ya mkutano huo na kupendekeza kwa pamoja wazo la "kuhimiza na kulinda haki za binadamu kwenye maendeleo".

    Katika mkutano huo mwenye kauli mbiu ya "mchango wa maendeleo kwa ajili ya kufurahia haki za binadamu", Balozi wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Chen Xu amesema, China siku zote inafanya maendeleo yake yaendane na maendeleo ya dunia, na kujitahidi kujiendeleza huku ikitimiza maendeleo ya pamoja. Mwaka jana, mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika mjini Beijing, na kupata mafanikio makubwa. Amesema China itaendelea kuhimiza pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na "Hatua Nane" kuunganisha na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali za Afrika, ili kuisaidia Afrika kuharakisha kubadilisha rasilimali zake kuwa msukumo wa maendeleo, na kuhimiza watu wa China na Afrika kutimiza haki mbalimbali za binadamu.

    Wajumbe waliohudhuria mkutano huo wamepongeza kufanyika kwa mkutano huo, na kusema maendeleo yanasaidia kuondoa umaskini, na kuinua kiwango cha maisha na maslahi ya watu. Pia wameishukuru China kwa kutoa msaada kwa nchi za Afrika, na kuitaka jumuiya ya kimataifa iendelee kuzisaidia nchi za bara hilo na nchi nyingine zinazoendelea kutimiza maendeleo, na kuhimiza na kulinda haki za binadamu wakati zinapojiendeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako