Mahakama kuu yadumisha adhabu ya kifo Tanzania
Mahakama Kuu ya Tanzania imesema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa hukumu ya kifo ni kinyume na katiba ya nchi.
Watetezi wa haki za binadamu walifungua kesi kutaka adhabu hiyo ifutwe kwani inakiuka haki ya msingi ya kuishi.
Hukumu hiyo haijatekelezwa tangu mwaka 1994. Wafungwa 500 wanakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha maisha.
Baada ya kuahirishwa kwa mara mbili mfululizo hatimaye majaji wa mahakama hiyo walitoa uamuzi wao kuhusu kesi hiyo ambayo iliwasilishwa na na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Tanzania wakitaka hukumu ya kifo ifutiliwe mbali. Hukumu hiyo iliyosomwa na jaji Benhajj Masoud imeeleza kwamba hukumu ya kifo itaendelea kuwepo kwa sababu ipo kikatiba.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |