• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchambuzi: China na Marekani hazitafikia makubaliano kama Marekani haitekelezi ahadi zake mara kwa mara

  (GMT+08:00) 2019-08-03 18:08:07

  Marekani hivi karibuni ilitumia tena fimbo ya ushuru ikisema kuanzia tarehe mosi, Septemba itaongeza ushuru wa asilimia kumi kwa bidhaa za China zinazouzwa nchini humo, huku ikieleza matumaini ya kufanya mazungumzo mazuri na China kuhusu kufikia makubaliano kamili ya biashara. Ni kweli baadhi ya wamarekani hawana mantiki, na kufuata ahadi ni msingi wa mazungumzo. Je, upande unaobadilisha msimamo wake mara kwa mara unaweza kuaminika?

  Katika mwaka mmoja uliopita na zaidi, China imejadiliana na Marekani kwa uaminifu na kwa udhati mkubwa, na mazungumzo yao yamepata maendeleo makubwa. Hata hivyo, Marekani ilikiuka maoni ya pamoja mara nne na kutofuata ahadi yake na kusababisha mazungumzo yakatike mara kadhaa.

  China siku zote inaona kuongeza ushuru hakusaidii utatuzi wa suala, na ni kupitia mazungumzo tu, ndipo migongano inaweza kutatuliwa. China haiogopi shinikizo na tishio lolote, na imejianda vya kutosha kukabiliana na changamoto yoyote. Kama Marekani itaongeza ushuru, China haina budi kuchukua hatua za kujibu ili kulinda maslahi yake na ya wananchi wake. Kama baadhi ya watu wa Marekani hawafuati ahadi zao mara kwa mara, mazungumzo hayatakuwa na matokeo mazuri bila ni jinsi gani pande mbili zinavyojitahidi kujadiliana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako