China imeanzisha taasisi 59 na madarasa 41 ya Confucius katika nchi 44 za Afrika hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, na kutoa nafasi za kujifunza lugha ya kichina kwa watu wa nchi hizo. Taasisi ya Confucius iliyopo katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya ilianzishwa mwezi Disemba mwaka 2005, na katika miaka 14 iliyopita imeandikisha wanafunzi zaidi ya elfu 15.
Msichana anayeimba anaitwa Wangui Ruth Njeri kutoka Kenya. Mwaka 2013, aliimba wimbo la kichina "Usiku Usioweza Kusahaulika" katika tamasha la sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina lililorushwa katika televisheni ya taifa ya China CCTV. Ruth aliongea vizuri kichina, na yeye ni mmoja kati ya wanfunzi wa mwanzo katika taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Pia aliwahi kujifunza katika chuo kikuu cha ualimu cha Tianjin kwa miaka minane na kupata shahada ya pili. Baada ya kurudi nyumbani, alikuwa mwalimu mzawa wa lugha ya kichina.
Alipozungumzia maarifa yake ya kujifunza kichina, Ruth alisema mwanzoni alitaka kujifunza lugha moja ya kigeni, lakini hakutarajia kuwa kichina kinaweza kubadilisha hatma yake. Ana matumaini kuwa vijana wengi wa Kenya wanaweza kujifunza kichina ili kubadisha hatma yao na ya taifa lao.
Anasema, "Nilianza kujifunza kichina katika taasisi ya Confucius mwaka 2005. Hivi sasa wakenya wengi wameanza kujifunza kichina katika taasisi ya Confucious. Nafikiri wao wanaona kuwa kujifunza kichina kunaweza kuboresha hatma zao, kwani uchumi wa China umekua kwa kasi na pia nchi hiyo ina utamaduni wa kina na wa historia ndefu."
Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Nairobi aliyosoma Ruth ni ya kwanza kuanzishwa barani Afrika. Taasisi hiyo ilianzishwa tarehe 19, Disemba mwaka 2005. Kwa mujibu wa mkuu wa taasisi hiyo upande wa China Xiao Shan, baada ya miaka kumi na zaidi, wanafunzi wanaoandikishwa wameongezeka hadi mia tano kutoka 20 kila muhula, na idadi ya jumla ya wanafunzi walioandikishwa imefikia elfu 15, na watu zaidi ya elfu 80 waliwahi kushiriki kwenye shughuli za kutangaza utamaduni wa China.
Anasema, "Tunaona fahari kuwa walimu wa taasisi za Confucius, na kwamba tumegundua kuwa wakenya wanazidi kutaka kujifunza kichina, na hamu hii kubwa inatokana na kuongezeka kwa nguvu ya taifa letu."
Katika miaka ya hivi karibuni, kwa kuhimizwa na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", China na Kenya zimezidi kuwasiliana kwa karibu katika mambo ya siasa, uchumi na utamaduni, na vijana wengi wameanza kujifunza kichina. Serikali ya Kenya imeamua kuwa, kuanzia mwaka 2020, wanafunzi wa shule ya msingi kuanzia darasa la nne na juu zaidi wataanza kujifunza kichina shuleni. Bibi Xiao Shan ameeleza kuwa, hivi sasa, taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Nairobi inashirikiana na kamati ya mageuzi na maendeleo ya masomo ya Kenya kutunga kwa pamoja mtaala wa masomo, na kubeba jukumu la kuandaa walimu wenyeji wa kichina. Hadi sasa kazi ya kutunga mtaala kwa wanafunzi wa darasa la nne na la tano imemalizika na inakaribia kutangazwa. Kwa mujibu wa mpango uliowekwa, majaribio ya kufundisha somo la kichina yatafanyika kuanzia mwaka 2020.
Kaimu mkuu wa chuo kikuu cha Nairobi ambaye pia ni mkuu wa taasisi ya Confucius upande wa Afrika Profesa Isaac Meroka Mbeche anaona kuwa, taasisi hiyo imesaidia sana katika kufundisha kichina na utamaduni wa China nchini Kenya na hata bara la Afrika, na kutoa mchango mkubwa katika kukuza urafiki kati ya watu wa China na Arika. Mbeche amesema wahitimu wengi wa taasisi ya Confucius wanafanya kazi muhimu katika sekta mbalimbali, baadhi yao wamekuwa wafanyakazi wa reli ya Mombasa-Nairobi, baadhi yao wameajiriwa na kampuni za China, na wengine wanafanya kazi katika idara za serikali zinazoshughulika na mambo ya nje. Amesema anapenda kuhamasisha vijana wengi kujifunza kichina na kuzindua mfumo wa "Kichina kujumuisha ufundi stadi"
Anasema, "Tumegundua kuwa taasisi ya Confucius imewavutia watu wengi kujifunza kichina, ambao wamekuwa walimu wa kichina na hata wanaendelea kusoma katika taaluma nyingine. Nimesisimka kwa kuona maendeleo haya."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |