Kutokana na mwaliko wa wizara ya afya ya Zimbabwe, timu ya 17 ya madaktari ya kuisaidia Zimbabwe ya China imeweka kibanda cha maonyesho ya dawa za jadi za Kichina kwenye Maonyesho ya Kilimo ya Zimbabwe ya mwaka 2019, ikiwa ni mara ya kwanza kwa bidhaa hizo kuonyeshwa kwenye maonyesho hayo.
Mke wa rais wa Zimbabwe ambaye pia ni balozi wa afya na watoto Bibi Auxilia Mnangagwa ametembelea kibanda hicho na kusifu ufanisi mzuri wa matibabu ya Akyupancha ya China, na kutumai kuwa China na Zimbabwe zitaimarisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta ya dawa za jadi ili kuwanufaisha watu wa Zimbabwe.
Wakati wa maonyesho hayo, kibanda hicho kinawavutia Wazimbabwe wengi kujaribu matibabu na kuuliza maswali, kuwapatia wenyeji ufahamu kuhusu dawa za jadi za Kichina na kuhimiza matumizi ya dawa hizo nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |