Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Ghana (GUTA) Bw. Joseph Obeng amesema, uhusiano wa kimakakti na China utachangia mafanikio ya Eneo la Biashara Huria barani Afrika (AfCFTA).
Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua mjini Accra, Bw. Obeng amesema tayari kuna uhusiano kati ya waagizaji bidhaa wa Afrika na watengenezaji wa China, ambao unaweza kutandika njia kwa watengenezaji hao kuwekeza barani Afrika. Amesema ushiriki wa China katika kuendeleza Eneo hilo utaongeza kasi ya mageuzi ya kiviwanda katika bara la Afrika na kujenga mazingira ya kunufaishana kwa pande zote mbili.
Bw. Obeng amesema, ukaribu wa manunuzi ya bidhaa kutoka nchi jirani ni mzuri sana, na hatua ya kuondolewa kwa vizuizi vya kibiashara inapaswa kupongezwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |