• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miji ikiwemo Cape Town yaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi duniani

    (GMT+08:00) 2019-09-02 08:32:38

    Mtaalamu wa mazingira wa Afrika Kusini Marian Nieuwoudt jana alisema, miji kando ya bahari ikiwemo Cape Town imeathiriwa na kuongezeka kwa kiwango cha bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, na wakazi wa sehemu kadhaa wanalazimika kupanga kuhamia kwenye sehemu za juu zaidi katika siku za baadaye.

    Nieuwoudt amesema, ufukwa wa eneo la Milnerton mjini Cape Town umeanza kuathiriwa. Eneo hilo limefanyiwa tathmini mara kadhaa na wataalamu wa mazingira kuhusu hatari ya kimazingira inayolikabili, pia watu wa sehemu hiyo wana uwezekano mkubwa wa kuhamia kwenye sehemu ya juu zaidi katika siku za baadaye.

    Nieuwoudt amezitaka serikali na jumuiya zinazohusika kuongeza uwekezaji na kulinda usalama wa wakazi na watalii kwenye maeneo ya pwani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako