Kwa mujibu wa Ripoti ya Ushindani wa usafiri na utalii TTCR, Afrika Kusini imekuwa moja ya nchi zinazoshika nafasi za mwanzo kwenye sehemu ya kusini mwa Sahara barani Afrika.
Ripoti hiyo iliyotangazwa jana ambayo inaorodhesha nchi 140 kwa nguvu zao za utalii na usafiri duniani, ilizinduliwa kando ya Mkutano wa Baraza la Uchumi Duniani kuhusu Afrika lililofanyika huko Cape Town. Ripoti hiyo pia imesema sehemu ya Afrika kusini mwa Sahara inatarajiwa kuwa ya pili kwa kiwango kikubwa cha ukuaji wa utalii katika miaka 10 ijayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |