Waziri wa Mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok ametangaza uundaji wa baraza la mawaziri la mpito, ambalo ni la kwanza tangu rais Omar al-Bashir kuondolewa madarakani.
Bw. Hamdok ametangaza uundaji huo katika mkutano na wanahabari uliofanywa huko Khartoum, huku akinukuu amri ya katiba iliyotolewa na mwenyekiti wa baraza la utawala.
Chini ya amri hiyo Bw. Hamdok amewateua mawaziri 18, lakini amechelewa kuwataja mawaziri wa wizara ya miundombinu na uchukuzi na wizara ya mifugo na uvuvi.
Bw. Jamal Omer ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi na Bw. Teraifi Idriss ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani, ambao wamependekezwa na kitengo cha kijeshi cha baraza la utawala.
Mawaziri hao 18 ni pamoja na wanawake 4, ambao miongoni mwao kuna waziri wa mambo ya nje wa kike wa kwanza wa nchi hiyo Bi Asma Mohamed Abdullah.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |