• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maktaba mapya ya UDSM yajengwa kwa msaada wa China

    (GMT+08:00) 2019-09-16 09:13:51

    China imetoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania kupitia uwekezaji, msaada na ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo. Mfano wa hivi karibuni wa mchango wa Uchina kwa Tanzania ni maktaba kubwa zaidi ya katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

    Maktaba ya UDSM inaweza kuhifadhi vitabu 800,000 na kuchukua watu 2,100 kwa wakati mmoja, pia ina ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa viti 600.

    Yohanna Matias mwanafunzi wa katika Chuo Kikuu cha Dar, hivi sasa ako mwaka wake wa tatu, na anasomea sheria.

    Ikiwa katika mwaka wa tatu katika chuo hichi inamaana alitumia maktaba ya zamani kabla ya hii mpya kujengwa.

    Matias anatueleza mabadilko makubwa ya liokuja na maktaba kubwa zaidi Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

    Maktaba hii ilijengwa na serikali ya China, lengo kuu likiwa kupiga jeki elimu za nchi za Afrika Tanzania ikiwa ya kwanza kufaidika na maoni hayo.

    Mbali na ujenzi wa maktaba kubwa Afrika Masharika na Kati , Tanzania imekuwa ikipokea misaada mingi katika miaka ya hivi karibuni kutoka kwa serikali ya China.

    Moja ya msaada mkubwa ya Uchina katika miaka ya hivi karibuni ni Jumba la Mkutano ya Kimataifa na ujenzi wake ni wa kisasa na ilipewa jina la Rais wa kwanza Baba wa Tanzania Julius Nyerere.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako