Habari kutoka Mkutano wa 5 wa baraza la uwekezaji barani Afrika uliofanyika mjini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo zinasema kuwa, mfuko wa maendeleo ya China na Afrika umewekeza dola za kimarekani bilioni 5 katika nchi 36 za Afrika, na kuhimiza kampuni za China kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 24 barani humo.
Mkutano huo liliandaliwa kwa pamoja na wizara ya fedha ya China, benki ya maendeleo ya China, serikali ya Jamhuri ya Kongo na benki ya dunia. Makubaliano ya miradi mbalimbali kati ya China na Afrika yamesainiwa kwenye mkutano huo, ambayo yanalenga kuimarisha zaidi ushirikiano na Afrika katika safari za anga, uzalishaji wa umeme, sekta ya viwanda, sekta ya fedha na kadhalika, na yatasaidia maendeleo endelevu ya uchumi wa Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |