Shirika la Afya Duniani (WHO) limezitaka mamlaka nchini Tanzania kutoa taarifa za matokeo ya vipimo vilivyofanywa hivi karibuni kuhusu kile kilichoelezwa kuwa ugonjwa wa ajabu uliosababisha vifo vya watu wawili nchini humo.
Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Shirika hilo imesema, uhaba wa taarifa rasmi kutoka mamlaka nchini Tanzania kunaleta changamoto katika kutathmini hatari zinazoletwa na ugonjwa huo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, waziri wa afya nchini Tanzania Bi. Ummy Mwalimu alikana fununu za mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo, na kuwataka wananchi wasiwe na hofu juu ya fununu hizo. Bi. Ummy alisema hayo baada ya kuzagaa kwa habari kupitia mitandao ya kijamii kuwa watu wawili wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola, ugonjwa ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 2 katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |