Sherehe ya uzinduzi wa ikulu mpya mjini Bujumbura, Burundi iliyojengwa kwa msaada wa China ilifanyika jana tarehe 27, na kuhudhuriwa na rais Pierre Nkurunziza na viongozi wengine wengi wa nchi hiyo.
Akitoa hotuba kwenye sherehe hiyo, rais Nkurunziza amesema China ni rafiki mkubwa zaidi wa Burundi na mradi huu wa ikulu umeonyesha uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa hii ni hatua muhimu iliyopigwa na taifa hilo kwani Burundi haitakuwa na haja ya kukodi mahali pa kufanyia shughuli za serikali, huku akitoa wito kwa raia wa Burundi kuongeza umoja na kupigania siku nzuri za baadaye.
Naye balozi wa China nchini Burundi Bw. Li Changlin amesema China siku zote inashirikiana na nchi za Afrika kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika iliyo na uhusiano wa karibu zaidi, na China inaichukulia Burundi kama rafiki wa wakati wote, na inapenda kutoa mchango wake kwa ajili ya maendeleo ya sekta mbalimbali za Burundi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |