Rwanda yatoa mwito wa uwajibikaji wa pamoja kupambana na wanaokanusha kutokea kwa mauaji ya halaiki
Mwenyekiti wa Baraza la Seneti la Rwanda Bw. Bernard Makuza amesema ni wajibu wa pamoja kwa vyombo vya habari na jumuiya nyingine kupambana na watu wanaojaribu kukanusha kutokea kwa mauaji ya halaiki au kuyafanya kama ni jambo dogo.
Akiongea baada ya kutolewa kwa ripoti kuhusu hali ya kukanusha mauaji ya halaiki, Bw. Makuza amesema watu wanaokanusha au kupuuza kutokea kwa mauaji hayo wamechagua njia ya teknolojia za kisasa, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii na vyombo vikubwa vya habari kueneza mawazo yao kutoka nje ya nchi.
Amesema vituo vya Radio na televisheni vinavyokanusha mauaji ya kimbari vimefunguliwa na wanyarwanda wanaoishi uhamishoni, lakini pia hufanya hivyo kwa kutumia vitabu na mijadala ya umma.
Ripoti hiyo pia imetoa mwito kwa serikali kuwahamasisha wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi kuwa na umoja na serikali na kushiriki kwenye programu za masikilizano, kama vile shughuli za kumbukumbu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |