• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36

    Ethiopia kurushiwa satelaiti ya kwanza mwezi Disemba kutokana na msaada wa China

    Rais Sahle-Work Zewde wa Ethiopia amesema satelaiti ya kwanza ya nchi hiyo inatarajiwa kurushwa mwezi Disemba mwaka huu chini ya msaada wa serikali ya China.

    Akizungumza kwenye kikao cha bunge kilichofunguliwa Jumatatu, rais Zewde amesema satelaiti hiyo ya ETRSS-1 yenye uzito wa kilo 70 itarushwa kutoka kituo cha kurushia satelaiti nchini China, na inatarajiwa kusaidia juhudi za nchi hiyo kutimiza malengo yake katika sekta za kilimo, misitu na uhifadhi wa maliasili.

    Baada ya kurushwa, satelaiti hiyo itadhibitiwa kutoka Kituo cha kuchunguzia anga cha Entoto kilichoko karibu na mji wa Addis Ababa, Ethiopia.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako