Kongamano la Kimataifa la Idadi ya Watu na Maendeleo ICPD25 lafunguliwa rasmi leo jijini Nairobi
Kongamano la Kimataifa la Idadi ya Watu na Maendeleo (ICPD25) lilikamilika alhamisi (tarehe 14 Nov) jijini Nairobi katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la KICC.
Lengo la kongamano hili ni pamoja na kutokomeza vifo vya mama na mtoto,kuhakikisha mahitaji yote ya uzazi wa mpango yanawafikia wahitaji na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kufikia mwaka 2030.
Baada ya miaka 25 hatimaye kongamano la ICPD25 lilifunguliwa rasmi tarehe 12 jijini Nairobi katika jumba la mikutano la KICC.
Kongamano hilo lilifanyika Cairo,Misri,miaka 25 iliyopita ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliazimia kupunguza na hatimaye kutokomeza vifo vya wajawazito,wanawake na watoto ili dunia iwe na ustawi kwa wote bila kujali mtu anaishi eneo gani.
Kongamano hili ambalo limeandaliwa na serikali za Kenya na Denmark kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Idadi ya Watu,ni la ngazi za juu,na linalenga kuhamasisha utashi wa kisiasa na ahadi za kifedha ambavyo vinahitajika ili kutekeleza kikamilifu mpango wa kongamano hili la kimataifa la idadi ya watu na maendeleo.
Kaimu Waziri wa Fedha wa Kenya Ukur Yattani amewahakikishia wajumbe wote kuwa matayarisho yamekamilika na usalama umeimarishwa.
"Tunapowakaribisha wajumbe watakaoshiriki kongamano hili hapa jijini Nairobi,ningependa kuwahakikishia ninyi na wao kuhusua utayari wa nchi wa kuwa mwenyeji wa kongamano la kufana.Hatua zote za kiusalama zimetimizwa kuhakikisha kuwa wajumbe wako salama na watafurahia muda wao katika kongamano hili"
Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Idadi ya Watu (UNFPA) Arthur Erken alisema kongamano hilo linalenga kusukuma ajenda ya wanawake.
"Tunataka kuhakikisha kupitia kongamano hili ,tunajitolea tena na kujifunga na ajenda ya kuwaweka wanawake katikati ya maendeleo,uwezeshaji wa wanawake na usawa kama vichocheo vya maendeleo endelevu.Na pia kuhakikisha kuwa tunafikia upatikanaji wa matibabu na afya ya uzazi kwa wote kama tulivyoahidi miaka 25 iliyopita jijini Cairo mwaka 1994"
Sambamba na mambo yaliyojadiliwa katika kongamano hili,ijumaa iliyopita Rais Kenyatta alizindua kampeni ya kupinga na kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana nchini kufikia mwaka 2022.
"Ukeketaji ulikita mizizi katika tamaduni za baadhi ya jamii zetu za Kenya,nafikiri itakuwa sawa na kweli kusema kwamba utamaduni huo nafasi tena katika jamii yetu ya Kenya"
Mkurugenzi wa Shirika la Umoja Mataifa la Mfuko wa Idadi ya Watu Arthur Erken amesema kongamano hilo litaangazia masuala ya ndoa za mapema pamoja na ukeketaji na mambo mengi yanayomhusu mwanamke.
"Nataka kuhakikishia kila mmoja kwamba kongamano hili linahusu kuokoa maisha.Kongamano hili linahusu wanawake 800 ambao wanakufa kila siku wakati wa kujifungua au wakati wa ujauzito.Kongamano hili linahusu wanawake robo bilioni ambao wangependa kutumia mbinu za kisasa za uzazi wa mpango lakini hawawezi kupata.Hii inahusu wasichana milioni 4 ambao kila mwaka wanakeketwa"
Kongamano hili linawaleta pamoja wajumbe kutoka nchi 160 kote duniani,linafunguliwa rasmi leo tarehe 12 Novemba na kukamilika tarehe 14 Novemba,2019.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |