Nguzo ya chuma cha pua ya Mnara mkuu kwenye Eneo la CBD mjini Cairo, Misri unaojengwa na kampuni ya ujenzi ya China CSCEC, imewekwa tayari kwa mara ya kwanza, hatua ambayo inamaanisha kuwa ujenzi wa mnara huo unaosifiwa kama jengo refu zaidi barani Afrika umeingia katika kipindi kipya.
Nguzo hiyo yenye uzito wa tani 26.8 ilipandishwa na kuwekwa kwenye msingi wa saruji ndani ya dakika kumi.
Imefahamika kwamba mnara huo wa eneo la CBD katika mji mkuu wa Misri, utakuwa na urefu wa mita 385.8, ghorofa mbili chini ya ardhi na ghorofa 78 juu ya ardhi, ambao utakuwa jengo refu zaidi barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |