• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China kuchimba udongo wa Diatomite nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-11-26 17:11:33

    Kampuni ya Kimataifa ya Madini ya Chuanshan ya China na serikali ya Kenya zimesaini makualibano ya kuchimba udongo wa Diatomite katika jimbo la Baringo lililoko kaskazini magharibi mwa Kenya. Maofisa wa Kenya wamesema mradi huu utahimiza maendeleo ya sekta ya viwanda na uchumi wa jimbo hilo.

    Jimbo la Baringo linajulikana kutokana na ziwa Baringo. Katika muda mrefu uliopita watu wa huko wameendesha maisha kwa kazi za kilimo na ufugaji. Miaka kadhaa iliyopita, udongo wa Diatomite unaotumiwa katika uhifadhi wa mazingira uligunduliwa, na kuleta matumaini mapya kwa watu hao. Naibu waziri wa mafuta na madini wa Kenya Bw. John Morangi anataka kubadilisha njia ya kuendesha maisha ya vijana wa jimbo hilo kupitia kuendeleza viwanda vya madini. Anasema,

    "Tuna maliasili kubwa ya madini. Tunatumai kuzichimba ili kuwashirikisha vijana wa jamii kwenye sekta ya viwanda badala ya kilimo na ufugaji."

    Udongo wa Diatomite unatokana na mabaki ya mwani aina ya Diatom ya zama za kale, na ni malighafi mpya ya kupambana nyumba ambayo haileti uchafuzi. Licha ya kupamba nyumba, udongo huo pia unatumiwa katika sekta ya vyakula, dawa na kemikali.

    Kampuni ya Kimataifa ya Madini ya Chuanshan kutoka mkoa wa Shandong, China imepata idhini ya kutafuta na kuchimba madini, hati ya uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia na hati ya matumizi ya ardhi nchini Kenya. Hadi sasa kampuni hiyo imemaliza kazi ya kutafuta madini, na itaanza kuzichimba. Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi na pia ni meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Han Ke anasema,

    "Udongo wa Diatomite haswa unatumiwa katika uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia. Nchini China haswa unatumiwa katika kushughulikia uchafuzi wa maji, hewa na ardhi. Tunautumia sana katika sehemu za kaskazini mashariki na kaskazini. Kwani hivi sasa China inazingatia uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia."

    Akiulizwa uchimbaji wa udongo huo utaweza kuleta uchafuzi wa mazingira ya kienyeji, Bw. Han amesema kutoka mwanzoni kampuni yake imefikiria kwa makini suala hilo, na baada ya kuchimba udongo huo watarudisha mchanga kwenye mashimo ya mgodi na kupanda miti na mimea mingine, ili kuhifadhi mazingira ya kiikolojia. Anasema,

    "Kwani udongo wa Diatomite ni maliasili ya kuhifadhi mazingira, hivyo hatuwezi kuleta uchafuzi. Tumeahidi kurudisha mchanga kwenye mashimo ya mgodi na kupanda mimea baada ya kuchimba udongo huo wakati tulipoomba mradi huo kwa wizara ya maliasili ya China na wizara ya mafuta na maliasili ya Kenya. Udongo utakaochimbwa pia utashindikwa jimboni Baringo, ili kuhimiza ongezeko la ajira na pato la jimbo hilo."

    Bw. Han amesema mradi huo unatarajiwa kuleta ajira 1,500 kwa jimbo la Baringo. Mbali na hayo, kampuni yake pia itajenga shule ya ufundi stadi na eneo la viwanda, ili kuhimiza maendeleo ya jimbo hilo.

    Mkuu wa jimbo la Baringo Bw. Stanley Kiptis amesema wanatumai mradi huo utapiga hatua, ili kuleta ajira na maendeleo ya pato la serikali. Anasema,

    "Kuendeleza sekta ya madini ni sehemu muhimu ya maendeleo ya viwanda. Serikali za Kenya na China zina uhusiano wa karibu. Tumeanzisha uhusiano wa kibalozi tangu mwaka 1963, na tumepata mafanikio mengi ya ushirikiano. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alitoa 'Ajenda Nne za Maendeleo', ambazo zitabadilisha jamii, uchumi na maisha ya Wakenya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako