Slovenia: Nyota wa Nigeria atimuliwa klabuni baada ya kumpa ujauzito mtoto wa rais wa timu
Mchezaji wa soka raia wa Nigeria jina lake halijawekwa wazi ametimuliwa na klabu yake inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Slovenia baada ya kumpa ujauzito binti wa rais wa klabu hiyo, ikiwa ni miezi sita tu imepita tangu asajiliwe na timu hiyo. Taarifa zinadai kuwa ililazimika kumfukuza mchezaji huyo kutokana na mwenendo mbaya na kitendo cha utovu wa nidhamu baada ya kumpa ujauzito mtoto wa rais.
Hata hivyo mchezaji huyo ameanza kuchukua hatua dhidi ya waajiri wake kwakua anaamini kitendo hicho ni cha kiuonevu.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini Ghana, Mchezaji huyo amekiambia chombo cha habari kwamba huku alisaini mkataba wa miaka mitatu huku mkataba wake ukiwa na kipengele cha kinamruhusu kuongeza mwingine.
Kuna wachezaji wanne tu wa Nigeria ambao wanacheza soka la kulipwa nchini Slovenia kwenye ligi la daraja la pili.
Bede Osuji, Temitope Nelson, Gerald Chiyoke na Sulaiman Adedoja ambao hawa wote hucheza Slovenia hivyo mpaka sasa bado haijafahamika ni yupi kati yao amehusika na kumpatia mimba binti huyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |