Mjumbe wa taifa wa China aliyeko ziarani nchini Lesotho Bw. Wang Yong jana alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Lesotho Bw. Thomas Motsoahae Thabane mjini Maseru.
Kwenye mazungumzo yao, Wang amesema uhusiano kati ya China na Lesotho unaendelea vizuri kwa utulivu katika miaka ya karibuni, pande zote mbili zinaheshimiana na kutendeana kwa usawa na hali ya kuaminiana ya kisiasa imeongezeka zaidi. China siku zote inaichukulia Lesotho kuwa ni rafiki na mwenza wake wa dhati, na inaipongeza Lesotho kwa kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja. Aidha amesema China inapenda kushirikiana na Lesotho katika kuimarisha muungano wa mikakati ya maendeleo, kupanua ushirikiano na mawasiliano ya watu, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea kwenye mambo ya kimataifa.
Naye Bw. Thabane amesema Lesotho inaishukuru China kwa kuunga mkono na kutoa msaada kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini humo. Lesotho inatilia maanani kuendeleza uhusiano na China, itashikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, kuimarisha hali ya kuaminiana ya kisiasa kati ya pande mbili, na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana kwenye sekta mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |