• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 11-Januari 17)

    (GMT+08:00) 2020-01-17 18:57:01

    Kiongozi mstaafu wa Kanisa Katoliki Papa Benedict wa 16 ametetea suala la makasisi kutofunga ndoa

    Kiongozi mstaafu wa Kanisa Katoliki Papa Benedict wa 16 ametetea suala la makasisi kutofunga ndoa wakati ambapo mrithi wake anafikiria kulegeza marufuku hiyo kwa wanaume wanaooa ambao wanahudumu kama makasisi.

    Papa Benedict amesema hayo katika kitabu walichoshirikiana na Kadinali Robert Sarah.

    Hatua hiyo inawadia kujibu pendekezo la kuruhusu wanaume waliooa kutawazwa kama makasisi katika eneo la Amazon.

    Papa Benedict, ambaye alistaafu mwaka 2013, amesema hakuweza kunyamazia suala hilo.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Katika kitabu hicho, Papa Benedict amesema kutofunga ndoa kwa makasisi ni utamaduni wa kale ambao umekuwepo kwa karne nyingi tu ndani ya kanisa hilo, una umuhimu mkubwa kwasababu unaruhusu makasisi kuangazia majukumu yao.

    Papa Benedict mwenye umri wa miaka 92 amesema Hilionekani kuwa jambo linalowezekana kutimiza majukumu ya ukasisi na ndoa kwa wakati mmoja.

    Vatican bado haijasema lolote kuhusu na kitabu hicho, ambacho kiliangaziwa kidogo katika gazeti la Ufaransa la Le Figaro kabla ya kuchapishwa leo Jumatatu.

    Wachambuzi wa Vatican wameshangazwa na hatua ya Papa Benedict kuingilia suala hilo, na kuongeza kwamba hatua ya Papa Benedict inavunja utamaduni ambao umekuwepo.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako