• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa kikundi cha madaktari wa China nchini Namibia Chu Hailin

    (GMT+08:00) 2020-01-24 18:12:49

    Leo ni mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa kichina. Wachina wana desturi ya kukaa pamoja na familia zao ili kusherehekea sikukuu hiyo. Lakini kwa madaktari Wachina wanaotoa msaada wa matibabu barani Afrika, leo ni siku ya kawaida ya kazi.

    Nchini Namibia, kuna kikundi cha madaktari wanne kutoka China, ambao wanatoa matibabu maalumu ya jadi ya kichina kwa Wanamibia. Bw. Chu Hailin ni kiongozi wa kikundi hicho, na amefanya kazi nchini Nambia kwa miaka sita.

    "Hii ni mara yako ya kwanza kuja hapa? Una miaka mingapi?"

    "Ndiyo, ni mara yangu ya kwanza, nina miaka 46."

    "Una shida gani?"

    "Naumwa na mgongo. Nilifanyiwa upasuaji mwaka 2013, na nimeendelea kuumwa mpaka sasa. Naishi Ondangwa, daktari mkuu wa hospitali ya huko alinishauri kuja hapa kupata matibabu."

    Saa mbili asubuhi, Bw. Kristof kutoka mji wa Ondangwa kaskazini mwa Namibia alifika kwenye kituo cha madaktari Wachina wa tiba ya vitobo yaani akupancha kwenye hospitali ya kitaifa ya Katutura. Bw. Chu alimpokea na kuanza kumtibu. Anasema,

    "Tuna wagonjwa wengi sana. Siku moja tuliwatibu wagonjwa 121, japo tuna madaktari wawili na wauguzi wawili tu."

    China imeanza kutuma kikundi cha madaktari kwenye hospitali ya Katutura nchini Namibia tangu mwaka 1996. Kikundi kilichoongozwa na Bw. Chu ni kikundi cha 12, na kuanzia tarehe 2 Juni mwaka 2018 hadi tarehe 31 Disemba mwaka 2019, madaktari wa kikundi hicho walitibu wagonjwa 22,509.

    Hii ni mara ya tatu kwa Bw. Chu mwenye umri wa miaka 52 kutoa msaada wa matibabu nchini Namibia. Uzoefu mkubwa wa kufanya kazi hii umemfanya afahamu vizuri majukumu ya daktari anayetoa msaada wa matibabu nje ya China. Anasema,

    "Hapa tuna wagonjwa wengi zaidi kuliko nchini China. Hali hii inamaanisha kuwa matibabu ya jadi ya kichina yanasaidia. Tukiwa madaktari wa kutoa msaada wa matibabu barani Afrika, tunatoa huduma bila ya malipo."

    Wanamibia waliowahi kutibiwa na kupata nafuu na madaktari hao kutoka China ni kutoka rais hadi raia wa kawaida. Kazi za madaktari hao zimepongezwa sana na Wanamibia. Bw. Constantin aliyetibiwa nao mara tano anasema,

    "Tiba ya akupancha ya China ni nzuri. Naridhika sana. Shauri langu ni kueneza tiba hiyo, ili Wanamibia wote wanufaike. Nilipokuja hapa, nilikuwa ninatembea kwa gongo, lakini sasa najisikia vizuri sana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako