Mkurupuko wa ugonjwa China. Usafiri wasitishwa Wahun, uwanja wa ndege na vituo vya treni kufungwa
China imefanya maamuzi magumu ya kusitisha usafiri wa umma hasa katika mkoa wa Wuhan, wenye idadi ya watu takriban milioni tisa, wakati wa mkurupuko wa virusi vya ugonjwa wa Corona.
Watu wanaoishi katika jiji hilo wameambiwa wasiondoke nje ya mji huo , na uwanja wa ndege na vituo vya treni vitafungwa kwa abiria wanaotoka nje ya eneo hilo.
Basi, reli za chini ya ardhi, feri, na mitandao ya uchukuzi wa umbali mrefu itasitishwa kuanzia leo Alhamisi.
Virusi vipya vimeenea kutoka Wuhan hadi majimbo kadhaa ya China, Marekani, Thailand na Korea Kusini.
Huku haya yakijiri, shirika la afy ulimwenguni WHO limesema maambukizi ya virusi mjini Wuhan hayajawa tukio la dharura la afya ya umma PHEIC
Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa maambukizi ya virusi vipya vya nimonia aina ya 2019-nCoV nchini China, hayajawa tukio la dharura la afya ya umma linalofuatiliwa na dunia PHEIC.
Mkutano wa dharura wa WHO uliofanyika Alhamisi umetangaza baada ya majadiliano, kuwa ni mapema kwa sasa kuyatangaza maambukizi hayo kuwa ni tukio la dharura la afya ya umma linalofuatiliwa na dunia, sababu kuu ni kwamba idadi ya watu wanaoambukizwa virusi hivyo nje ya China ni wachache, na serikali ya China imetekelezwa hatua madhubuti za kinga na udhibiti.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |