• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi wa SGR Kenya wachanga pesa kwa mapambano ya China dhidi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-06 20:26:42

    Kampuni inayosimamia uendeshaji wa reli ya SGR ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, Kenya ilifanya shughuli ya kuchangisha pesa kwa ajili ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona nchini China. Licha ya wafanyakazi Wachina, Wakenya zaidi ya 180 pia wamechanga pesa ili kuipa moyo China.

    Awali, shughuli hiyo ilitangazwa kwa wafanyakazi Wachina pekee, lakini baada ya wafanyakazi Wakenya kuijua, wengi walieleza nia ya kushiriki. Naibu meneja wa kitengo cha usafiri wa abiria cha kampuni hiyo Bibi Dinah Waithira Kimani ni mmojawapo, na alichangia Shilingi elfu tano za Kenya.

    "Nilipopewa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa reli, kwa bahati nilitembelea mji wa Wuhan. Wuhan ni mji mzuri sana. Nilipoona mji huo umekumbwa na mlipuko wa virusi, niliguswa sana na kuelewa jinsi wanavyojisikia watu na familia zinazoathiriwa. Ndio maana, nataka kutoa mchango wangu kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo."

    Wuhan si mahali pageni kwa wafanyakazi wengi wa Kenya. Wengi wao waliwahi kwenda Wuhan kupata mafunzo. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Sammy Gachuhi ana hisia nzito na Wuhan. Alichangia Shilingi elfu 20 za Kenya. Amesema baada ya kuona hatua kabambe zinazochukuliwa na serikali ya China katika kudhibiti virusi, anaamani kuwa China itashinda mapambano hayo. Anasema,

    "Vitendo vinavyofanywa na serikali ya China vinatupa moyo mkubwa, na ndani ya siku kadhaa tu imejenga hospitali. Naamini kuwa baada ya muda mfupi virusi vya korona vitaweza kudhibitiwa na maisha yatarudi kwenye hali ya kawaida."

    Kutokana na mlipuko wa virusi vya korona, baadhi ya watu wana uelewa mbaya na ubaguzi dhdi ya China. Akizungumzia hilo, naibu mkuu wa safari za treni za abiria wa kampuni hiyo Bibi. Winfred Ndanu Mutua anasema,

    "Naona ni kosa kubwa sana. Sisi wote ni sawa bila kujali rangi tofauti za ngozi. Safari hii, virusi vimetokea China, pengine kesho vitatokea Afrika. Kama binadamu, unachopaswa kufanya ni kuwaunga mkono, na kuonesha mapenzi yako."

    Kutoka Mombasa, Nairobi hadi Naivasha, fedha zinachangiwa katika vituo mbalimbali vya reli ya Mombasa-Nairobi na Nairobi-Malaba yenye urefu wa kilomita 600. Ndani ya siku chache, wafanyakazi wa China na Kenya wamechangia dola za kimarekani karibu elfu 33. Meneja mkuu wa kampuni inayosimamia uendeshaji wa reli ya Mombasa-Nairobi Li Jiuping amesema, kampuni haikuhamasisha mtu yeyote kushiriki kwenye shughuli hiyo, watu walichanga pesa kwa hiari. Pia ametoa shukrani haswa kwa wafanyakazi wa Kenya.

    "Nchini China, madaktari, wauguzi na wengine wengi wamejituma kushiriki kwenye mapambano dhidi ya virusi vya korona. Sisi tukiwa nchi za nje wakati wowote tunajua taifa letu linatujali, naona kuchangia pesa kunaweza kueleza mapenzi yetu kwa taifa letu. Cha muhimu zaidi ni kuwa tunatakiwa kuendesha vizuri reli ya Mombasa hadi Nairobi na kuongeza idadi ya abiria na mizigo ili kuchangia maendeleo ya uchumi wa Kenya na urafiki kati ya China na Kenya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako