• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema hakuna raia kutoka Afrika aliyeambukizwa virusi kwa korona nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-02-14 16:35:18
    Balozi wa China nchini Kenya Wu Peng amesema hapana kisa chochote cha maambukizi ya virusi vya Corona kilichoripotiwa miongoni mwa Waafrika walio nchini China.

    Akitoa habari za hivi punde kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini China, Balozi Wu alitoa wito kwa Wakenya na raia wengine kutoka Afrika wanaoishi au kusomea nchini China kuwa watulivu, huku akisema "wako salama mahali walipo badala ya kuwahamisha."

    Balozi huyo alisema hii itasaidia kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo. Kulingana na Wu, China ina uwezo kitaaluma na uwezo wa rasilimali ya kuweza kushugulikia masuala yote ya dharura ya afya ya umma na kuhakikisha ufanisi.

    "Ni kawaida kuona baadhi ya watu walio nchini China pamoja na familia zao wakiwa na wasiwasi wakati huu mgumu. Lakini jambo la busara, salama, na linalofaa kwa wanafunzi wa Kenya na raia wengine ni kubakia mkoani Wuhan na China kwa muda. " Balozi Wu aliwaambia waandishi wa habari katika hoteli moja jijini Nairobi

    "Harakati za haraka haraka za kuwaondoa raia kutoka China huenda zikazidisha hofu." Aliongeza bwana Wu.

    Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na hofu kuhusu hali kamili ya wale ambao kwa wakati huu wako nchini China kufuatia kuzuka kwa virusi vya Korona ambavyo kufikia sasa vimesababisha vifo vya watu wengi na kuwaambukiza wengine wengi.

    Hata hivyo akitoa ripoti ya hivi punde kuhusu hali ilivyo nchini China, balozi wa nchi hiyo nchini Kenya Wu Peng amesema hapana haja ya kuwa na wasi wasi.

    "Ninaelewa kikamilifu wasiwasi na hofu ya familia za Wakenya wanaoishi au kusoma nchini China, hasa katika jiji la Wuhan. Ningependa kusisitiza kwamba, raia wa kigeni wakiwemo Kenya na Afrika nzima wako salama nchini China. " Wu alisisitiza

    Huku miito yakitolewa na watu kutoka mataifa mbali mbali za Afrika na ulaya kushinikiza kuondolewa kwa raia wao walio nchini China, ubalozi wa China umeshauri kwamba hatua kama hiyo ni hatari.

    "Kwa mujibu wa tathmini ya kitaalamu ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros Adhanom, njia salama zaidi kwa raia wa kigeni katika Wuhan ni kuendelea kubakia huko na kuhakikisha usalama wao." Alibainisha.

    Kulingana na balozi huyo, visa kadhaa vya maambukizi ya virusi hivyo vimethibitishwa miongoni mwa baadhi ya raia wa kigeni waliohamishwa kutoka nchini China.

    Anasema serikali ya China imeimarisha juhudi za kukabiliana na virusi hivyo na kwamba kushughulikiwa na kutibiwa kwa raia wa kigeni walio nchini China kimepewa kipaumbele.

    "Tunajaribu tuwezavyo kutoa huduma nzuri za matibabu, bidhaa za kila siku na msaada wa kila aina kwa wageni. Vyuo vikuu vyote nchini China sasa vimechukua hatua kuhakikisha vyuo hivyo vimezuiwa kutokana na janga hilo. " Alisema

    Balozi huyo alisema katika juhudi hizo, raia wa China wanaosafiri kutoka nchi hiyo wanatakiwa kujitenga kwa kipindi kisichopungua siku 15 kama sehemu ya mapambano dhidi ya virusi hivyo vya korona.

    Hakikisho hilo la Wu limewadia huku serikali ya Kenya likipongeza serikali ya China kwa juhudi zake za kukabiliana na ugonjwa huo, hasa kuhakikisha wanafunzi wa Kenya walio katika kitovu cha mchipuko wa ugonjwa huo wako salama na buheri wa afya.

    Wizara ya afya imehakikishia umma kwamba serikali ya Kenya inafanya kazi pamoja na taasisi zingine kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na virusi vya Corona.

    Kufikia alhamisi jumla ya visa 59,885 vya maambukizi ya virusi hivyo vilikuwa vimeripotiwa huku vifo 1,368 vikiripotiwa, na watu 6,000 kufikia sasa wametibiwa virusi hivyo na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako