• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatimiza kivitendo ahadi za kupunguza uchafuzi wa mazingira

    (GMT+08:00) 2020-02-15 19:35:52

    Mjumbe wa Baraza la Taifa la China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China ilitekeleza jukumu muhimu katika kuwezesha kusainiwa kwa mkataba wa mwisho wa Paris, na itatimiza ahadi zake kwa asilimia 100 kukabili mabadiliko ya tabianchi.

    Akihojiwa na shirika la habari la Reuters, Bw. Wang amesema, China ni nchi kubwa inayoendelea, na mchakato wa ukuaji wa viwanda bado haujakamilika, akiongeza kuwa ni muhimu kuharakisha mchakato wa maendeleo ili watu wa China waweze kuishi maisha bora.

    Wakati huo huo, alisema ikiwa nchi kubwa, China iko tayari kutekeleza majukumu yake ya kimataifa, kama inavyotakiwa. Alisema kwa nchi yenye idadi ya watu bilioni 1.4, kutimiza ahadi zake za kupunguza utoaji wa hewa chafu ni mchango mkubwa kwa ulimwengu na maendeleo ya watu kote duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako