Gavana wa benki kuu ya Zimbabwe RBZ Bw. John Mangudya, amesema, mchakato wa nchi hiyo wa kusitisha matumizi ya dola za kimarekani ulioanzishwa mwaka jana unaendelea kwa utaratibu.
Mwezi Juni mwaka jana serikali ya nchi hiyo ilitangaza kusitisha matumizi ya sarafu za kigeni ikiwemo dola za kimarekani. Mwezi Novemba iliidhinisha matumizi ya sarafu mpya nchini humo na kukomesha hali ya ukosefu wa sarafu za nchi hiyo katika miaka 10 iliyopita.
Bw. Mangudya amesema, hivi sasa uchumi wa nchi hiyo unafufuka huku kiwango cha mfumuko wa bei kikizidi kupungua hatua kwa hatua, hali ambayo itachangia kuweka mazingira mazuri zaidi ya kiuchumi kwa ajili ya mchakato wa kuondoa matumizi ya dola za kimarekani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |