Zimbabwe imepunguza ukubwa wa mashamba yote ya kibinafsi katika mikoa mitano ya kiikolojia, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha watu wengi zaidi wanapata ardhi.
Kupunguzwa kwa ukubwa wa mashamba pia kutaongeza utumiaji wa ardhi kufuatia wasiwasi kwamba, baadhi ya mashamba yalikuwa makubwa lakini hayatumiki ipasavyo.
Serikali ya Zimbabwe ilichukua zaidi ya hekta milioni 12 za ardhi ya kulima iliyokuwa inamilikiwa na raia wa nchi za magharibi, lakini hata hivyo wenyeji walijipatia maeneo makubwa ya ardhi hawakuweza kuyatumia vizuri.
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amekuwa akisema, mara tu ripoti kamili ya ukaguzi wa ardhi itakapotolewa, serikali yake itachukua shamba hizo na kuzigawanyia wengine wanaohitaji ardhi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |