• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Afrika Kusini asema Marekani haina uwezo wa kupambana na virusi vya korona kama inavyofanya China

    (GMT+08:00) 2020-02-20 20:07:21

    Balozi wa China nchini Afrika Kusini Bw.Lin Songtian amesema China imeonesha mfumo wake bora wa kipekee wa kisiasa haswa katika vita dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona COVID-19. Balozi Lin ametoa kauli hiyo kufuatia shutuma zilizotolewa hivi karibuni na waziri wa mambo ya nje wa Marekani dhidi ya mfumo wa kisiasa wa China, na kuongeza kuwa Marekani haiwezi kufanya vizuri kama inavyofanya China katika mambo kadhaa.

    Kwanza, chini ya uongozi wa katibu mkuu Xi Jinping na Chama cha Kikomunisti cha China CPC, wananchi wa China wameshikamana na kuzuia virusi vipya vya korona kuenea ndani na hata nje ya China ndani ya muda mfupi. Pili, China imejenga hospitali mbili maalum za magonjwa ya kuambukiza zenye vitanda 2,600 ndani ya siku kumi, pamoja na hospitali 15 za muda zenye vitanda zaidi ya elfu kumi. Tatu, wachina bilioni 1.4 wanafuata maelekezo ya CPC na serikali kuu kubaki majumbani kwao kwa hiari, jambo ambalo limekatiza kwa ufanisi uwezekano wa kuenea kwa virusi. Nne, China imehamasisha madaktari na wauguzi zaidi ya elfu 32 kutoka miji na mikoa mbalimbali kwenda na kuungana na wenzao wa Wuhan na miji mingine ya mkoa wa Hubei katika vita dhidi ya maambukizi ya virusi. Tano, China imetumia sera ya kuungana kati ya mikoa 19 na miji 16 isipokuwa Wuhan mkoani Hubei na kushiriki kwa pamoja katika vita hiyo. Sita ni kuwa, serikali kuu ya China na serikali za mitaa zimechukua hatua za haraka na kutenga dola za kimarekani bilioni 10 kuhakikisha fedha na vitu vinapatikana katika sehemu zenye mahitaji wakati huu wa vita dhidi ya virusi. Saba ni kuwa, CPC imefanikiwa kuwaondoa watu milioni 800 kwenye umaskini uliokithiri ndani ya miaka 40, na inajitahidi kuwawezesha wachina wote bilioni 1.4 kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ili kuchangia shughuli za kupunguza umaskini duniani. Nane ni kuwa, chini ya uongozi wa CPC, China siku zote inafuata njia ya kujiendeleza kiamani, kuishi kwa amani na nchi nyingine, haijawahi kuanzisha vita yoyote ya uvamizi kwa nchi za nje, haijawahi kukalia hata sehemu ndogo ya nchi nyingine, na haijamfanya raia yeyote wa kigeni kupoteza makazi.

    Balozi Lin amesema, Bw. Mike Pompeo akiwa waziri wa mambo ya nje wa nchi pekee yenye nguvu kubwa kabisa duniani, katika kipindi muhimu ambapo watu wa China wanapambana na maambukizi ya virusi, alipaswa kuonesha huruma na uungaji mkono kwa serikali ya China na watu wake kwa niaba ya serikali na watu wa Marekani, lakini alishambulia mfumo wa kisiasa wa China kwa makusudi mabaya, kitendo ambacho sio cha kiungwana wala maadili. Amesisitiza kuwa Marekani inaweza kufuata njia yake, lakini haitakiwi kulazimisha nchi nyingine kwani hakuna mfano hai kwamba nchi zozote zinazoendelea zikiwemo nchi za Afrika zimefanikiwa katika kunakili mfumo wa kimarekani.

    Balozi Lin anasema zama zimebadilika, dunia imebadilika na China pia imebadilika, na viongozi wa Marekani bora wajiangalie kwanza kabla kumsemea mwingine ili wasijiaibishe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako