• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema athari ya maambukizi ya virusi vya korona kwa biashara ya kigeni ni ya muda

    (GMT+08:00) 2020-02-21 18:09:45

    Wizara ya Biashara ya China imesema maambukizi ya virusi vya korona COVIC-19 yameiletea changamoto kubwa biashara ya China na nje, lakini athari hii itakuwa ya muda.

    Mkuu wa idara ya biashara ya kigeni ya Wizara hiyo Li Xingqian amesema, athari hiyo ni mbaya kiasi gani kwa biashara ya China na nje itaamuliwa na muda wa kuendelea kwa maambukizi hayo na maeneo yanayoathiriwa. Kwa mujibu wa tathmini ya sasa, athari mbaya kwa biashara katika robo ya kwanza ya mwaka huu itakuwa kubwa, lakini bado inaweza kuvumiliwa. Ili kupunguza zaidi athari mbaya kwa biashara ya China na nje, Wizara ya Biashara ya China imetoa mfululizo wa sera na hatua za kuunga mkono kampuni zinazofanya biashara na nchi za nje, kuzisaidia kuanza tena uzalishaji mapema, kuongeza kiwango cha kufuata mikataba, na itatoa sera zaidi baadaye.

    Li Xingqian amesema, China ina imani na mustakbali mzuri wa uuzaji na uagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi kwa mwaka huu mzima, kwani mahitaji katika soko la kimataifa ni tulivu na msingi wa kuendelea kwa biashara ya China na nje pia haujabadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako