Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemteua kiongozi wa kundi la upinzani Bw. Riek Machar kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Rais Kiir ametangaza amri ya Rais kupitia televisheni kumteua Bw. Machar, pamoja na manaibu rais watatu.
Taarifa imesema baraza la mawaziri litateuliwa leo, ambayo ndio siku ya mwisho ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Uamuzi huo unakuja baada ya Rais Kiir kurudi nyuma kwenye mvutano kuhusu idadi ya majimbo, suala lilikokuwa chanzo kikubwa cha tofauti na kundi la upinzani linaloongozwa na Bw. Machar. Idadi ya majimbo imepunguzwa kutoka 32 hadi kumi, hatua inayotajwa kuwa ni muhimu katika kuhimiza mchakato wa kisiasa.
Mbali na hatua hiyo, jumla ya wanajeshi elfu 38 kutoka upande wa serikali na upinzani wanapewa mafunzo, yatakayowawezesha kuchukua jukumu la usalama katika kipindi cha mpito cha miaka mitatu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |