Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Nairobi ikishirikiana na klabu ya wakenya waliosoma nchini China kimefanya hafla ya kuunga mkono juhudi za China katika kupambana na maambukizi ya COVID-19. Wasomi kutoka sehemu mbalimbali za Kenya waliosoma nchini China na Wakenya watakaokwenda China kwa masomo wametoa kauli ya kuunga mkono mapambano hayo nchini China.
"Tuko pamoja kukabiliana na maambukizi ya COVID-19!"
Watu zaidi ya 70 kutoka taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Nairobi na klabu ya Wakenya waliosoma nchini China wameshiriki kwenye hafla hiyo. Mwenyekiti wa klabu ya wakenya wanaoishi nchini China ambaye pia ni naibu mkuu wa mamlaka ya viwango ya Kenya Bw. Henry Rodichi amesema, hivi sasa idadi ya wagonjwa wapya waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo inaendelea kupungua, ikimaanisha kuwa hatua za mfululizo zilizochukuliwa na China ni sahihi na zenye ufanisi. Anasema,
"Ninachotaka kusema ni kuwa bila kuja jinsi msimu huu wa baridi unavyokuwa nchini China, majira ya mchipuko yatakuja. Bila kujali jinsi hali ya maambukizi inavyokuwa mbaya, madaktari wataishinda, na watu kote duniani watafanya juhudi ya pamoja kupata ushindi. Tunatarajia siku ambayo maambukizi yataisha, natarajia kwenda tena China."
Hivi sasa, wanafunzi karibia 90 kutoka Kenya wanaishi na kusoma mjini Wuhan, China. Bw. Aballah anayesoma shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Wuhan, pia ametuma video akisema,
"Sisi wanafunzi wa kigeni hapa Wuhan tuko salama na tuna afya nzuri. Maambukizi haya yataisha, na kila kitu kitarejea katika hali ya kawaida. Kwa sababu serikali ya China ina uwezo na imani ya kushinda vita hiyo."
Balozi mdogo wa China huko Nairobi Bw. Wang Xuezheng amesema, mlipuko wa COVID-19 ni changamoto kubwa. Ametoa shukrani kwa jumuiya ya kimataifa hasa watu wa Afrika kwa kuiunga mkono China katika mapambano dhidi ya maambukizi hayo. Anasema,
"Binadamu ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na virusi havina mipaka ya mataifa. Hadi sasa, viongozi kutoka nchi na mashirika zaidi ya 160 ya kimataifa wameeleza uungaji mkono wao. Serikali na watu kutoka makumi ya nchi wametoa misaada. Tunashukuru kwa dhati vitendo hivyo vvya kibinadamu"
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |