• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika Kusini mwa Sahara zarekodi maambukizi zaidi ya 100 vya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-17 09:42:52

    Idadi ya maambukizi ya nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona imezidi 100 katika Eneo la Afrika Kusini mwa Sahara, ambako nchi zaidi ya 20, zikiwemo Afrika Kusini, Nigeria na Ethiopia, zimeripoti visa vya maambukizi na kuchukua hatua kupambana na ugonjwa huo.

    Kati ya nchi za Afrika Kusini mwa Sahara, Afrika Kusini imeshuhudia ongezeko la kasi zaidi la idadi ya maambukizi tangu mtu wa kwanza kiliporipotiwa Machi 5, na mpaka Jana Jumatatu, watu 62 wamethibitishwa kuambukizwa COVID-19, wengi wao wakitoka Ulaya na Amerika Kaskazini.

    Mpaka Machi 12, wataalamu 62 wa Shirika la Afya Duniani WHO wametumwa katika nchi 18 za eneo hilo zenye maambukizi ya COVID-19, ambao wanatarajiwa kuzisaidia serikali za nchi hizo kuzuia na kudhibiti maambukizi zaidi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako