Wakati Kenya imethibitisha mtu wa nne kuambukizwa virusi vya Korona, ambaye aliwasili Kenya tarehe 9 Machi kutoka Uingereza, Balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng amesema China itachangia uzoefu na vifaa kwa nchi za Afrika katika kupambana na maambukizi ya COVID-19.
Bw. Wu Peng amesema Serikali ya China imetoa vitendanishi elfu 10 vya kupima virusi vya korona kwa kituo cha udhibiti wa maradhi cha Afrika. Na Kenya imepata baadhi ya vitendanishi vya upimaji kupitia njia hiyo, ambayo vimetoa mchango mkubwa katika kupunguza shinikizo la mahitaji ya vifaa vya upimaji. Kwa sasa China pia inashirikiana na baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Kenya katika utoaji wa vifaa vya kinga na udhibiti wa maambukizi ya COVID-19.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |