Mradi wa kukarabati hospitali ya kutibu virusi vya Corona ya Wilkins ya Zimbabwe uliofadhiliwa na kutekelezwa na kampuni ya China umekamilika na kukabidhiwa rasmi jana Jumatatu.
Hospitali hiyo mwanzoni mwa mwezi huu iliteuliwa kama kituo cha karantini na tiba ya ugonjwa wa COVID-19 huko Harare. Mradi huo wa kuinua kiwango cha hospitali ulianzishwa tarehe 13 na kukamilika tarehe 30 na kukabidhiwa kwa upande wa Zimbabwe. Baada ya mradi kukamilika, miundombinu ya hospitali hiyo na mazingira ya matibabu yameboreshwa na uwezo wake wa kuwatibu wagonjwa umeongezeka.
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa shukrani kwa msaada uliotolewa na serikali ya China na kampuni za China kwa nchi hiyo. Kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo, waziri wa afya wa Zimbabwe Bw. Obadiah Moyo pia ametoa shukrani kwa kampuni za China kutoa fedha kwa mradi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |