Vifaa vingi vya matibabu vilivyochangiwa na Mfuko wa Jack Ma na Mfuko wa Alibaba kutoka China, ikiwemo mask, vitendanishi, nguo na miwani ya kujikinga, vinasambazwa kwa nchi zote za Afrika.
Mchango huo unapokelewa wakati idadi ya vifo vinavyotokana na mlipuko wa COVID-19 barani Afrika imezidi 170 na maambukizi zaidi ya elfu tano yamethibitishwa.
Umoja wa Afrika umesema uwezo wa Afrika wa kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona umeinuka kidhahiri, baada ya kupata michango hiyo ya vifaa vya matibabu. Kutokana na misaada ya kimataifa, nchi za Afrika zilizoathiriwa na mlipuko wa COVID-19 zinachukua hatua mbalimbali za kuzuia kuenea kwa virusi, ambavyo vinatoa changamoto kubwa kwa bara hilo ambalo nchi nyingi zina mifumo dhaifu ya huduma za afya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |