Shirikisho la Soka Duniani FIFA linataka kuongeza umri kwa wachezaji wanaoshiriki mashindano ya soka ya Olimpiki ya Tokyo 2020, hapo mwakani kutoka miaka 23 hadi 24. FIFA imependekeza kubadilisha umri wa mwisho ili kuwaruhusu wachezaji waliokuwa wanatarajia kucheza michuano ya Olimpiki ya mwaka huu ambayo imeahirishwa kutokana na mlipuko wa virusi Corona. Wachezaji waliozaliwa Januari 1 1997 au baada ya hapo wataruhusiwa kucheza na FIFA. Mashindano ya wanawake katika Olimpiki ya mwakani hayatakuwa na ukomo wa miaka. Wakati huohuo FIFA imependekeza kufuta michuano yote ya kimataifa ya wanawake na wanaume iliyopangwa kufanyika June 2020 kwa sababu ya msukosuko unaoendelea duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |