Nchi mbalimbali za Afrika zimepunguza makadirio ya ongezeko la uchumi la mwaka huu kwa kiasi kikubwa kutokana na athari mbaya ya uenezi wa kasi wa virusi vya Corona kwa uchumi wa Afrika. Wachambuzi wanaona kuwa, mfumo wa afya na matibabu barani Afrika ni dhaifu, muundo wa uchumi ni rahisi na usio na unyumbufu , hivyo maambukizi ya virusi hivyo yataleta changamoto kubwa kwa uchumi wa Afrika.
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema, athari hiyo inaonekana katika sehemu tatu, kwanza ni hasara ya kifedha ya moja kwa moja kutokana na nchi za Afrika kuchukua hatua za kukinga na kudhibiti maambukizi hayo, pili ni kwaba maambukizi ya virusi hiyo yanaenea dunia nzima na kusababisha upungufu wa mahitaji, kusitisha utoaji, na mazingira magumu ya uvutiaji wa mitaji, mambo yatakayozorotesha uchumi wa Afrika, na tatu, bei ya bidhaa kuu imeshuka na kusababisha upungufu wa mapato ya uuzaji bidhaa muhimu haswa mafuta barani Afrika.
Aidha, nchi mbalimbali zimetenga fedha zaidi kwa mambo ya umma, na kuongeza zaidi shinikizo la kifedha. Wachambuzi wanaona kuwa ili kukabiliana na maambukizi hayo, nchi za Afrika zitaongeza matumizi ya fedha katika matibabu, wakikadiria kuwa zaidi dola za kimarekani bilioni 10.6 zitaongezwa.
Kutokana na athari ya maambukizi ya virusi vya Corona, Benki Kuu za nchi kadhaa za Afrika zimepunguza makadirio ya ongezeko la uchumi la mwaka huu. Makadirio ya ongezeko la uchumi la Kenya yamepungua na kuwa asilimia 3.4 kutoka 6.2 iliyokadiriwa awali. Uchumi wa Afrika Kusini umekadiriwa kupungua kwa asilimia 0.2, ongezeko la uchumi la Ghana limekadiriwa kupungua na kuwa asilimia 5 kutoka asilimia 6.8 iliyokadiriwa awali, na huenda ikafikia asilimia 2.5.
Mawaziri wa fedha wa nchi za Afrika waliohudhuria mkutano uliofanyika hivi karibuni kwa njia ya video walitoa wito kwa mashirika ya mikopo ya kimataifa kutoa msaada wa dharura kwa nchi za Afrika, ili kupunguza athari ya maambukizi ya virusi hiyo kwa uchumi na jamii barani humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |