Ronaldinho Gaucho ameachiwa kwa dhamana kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa kwa siku 32 kwa kosa la kuingia nchini humo na passport bandia. Passport ya nyota huyo wa zamani wa Brazil aliyoitumia kuingia nchini Paraguay, inaonyesha majina yake sahihi, mahali alipozaliwa, tarehe ya kuzaliwa, lakini inaonyesha kwamba ni raia wa Paraguay, badala ya Brazil. Ronaldinho hataruhusiwa kuondoka nchini Paraguay mpaka kesi yake itakapomalizika. Ronaldinho aliwahi kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mwaka 2004 na 2005, na alichezea timu za FC Barcelona na AC Milan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |