New York sasa ina visa vingi vya virusi vya corona zaidi ya taifa lolote duniani
New York sasa ina visa vingi vya virusi vya corona zaidi ya taifa lolote duniani, kulingana na takwimu mpya.
Serikali imethibitisha kwamba idadi ya visa vya ugonjwa huo imeongezeka kutoka 10,000 siku ya Alhamisi hadi 159, 937 na kuiweka mbele ya Uhispania ilio na visa 153,000 na Itali ilio na visa 143,000.
China ambapo virusi hivyo vilianza mwaka uliopita iliripoti visa 82,000. Marekani yote imerekodi visa 462,000 na takriban vifo 16,500. Huku duniani kote kuna takriban visa milioni 1.6 na vifo 95,000.
Operesheni za mazishi katika eneo hilo zimeongezeka kutokana na mlipuko wa virusi kutoka siku moja kwa wiki hadi siku tano kwa juma, kulingana na Idara magereza.
Ikulu ya Whitehouse ilikuwa imesema kwamba huenda Wamarekani milioni 2.2 wakafariki kutokana na virusi vya corona iwapo hatua hazitachukuliwa.
Agizo la kusalia nyumbani wakati huohuo limefunga biashara zisizo muhimu katika majimbo 42 huku likipunguza kasi ya uchumi wa taifa hilo.
Data mpya siku ya Alhamisi ilionyesha ukosefu wa ajira uliongezeka hadi milioni 6 kwa wiki ya pili mfululizo , ikiongeza idadi ya Wamarekani ambao hawako kazini katika kipindi cha wiki tatu zilizopita kufikia milioni 16.8.
Wakati huohuo Chicago imeweka amri ya kutouzwa kwa pombe kuanzia saa tatu siku ya Alhamisi ili kuzuia ukiukaji wa marufuku ya kupiga marufuku mikutano ya watu wengi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |