• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchambuzi wa kina watolewa na gazeti la Uganda kuhusu tukio lililowahusu raia wa Afrika huko Guangzhou

    (GMT+08:00) 2020-04-14 18:26:30

    Hivi karibuni, taarifa nyingi zilizagaa kuhusu ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa Afrika mjini Guangzhou, mji wenye idadi kubwa ya Waafrika, wakati China ikizingatia sana kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona kutoka nje. Lakini kufuatia mahojiano yaliyofanywa na gazeti la Daily Monitor la Uganda katika toleo lake la kila jumapili la Sunday Monitor, imegundulika kwamba, wahusika wengi waliodai kubaguliwa ni Waafrika ambao hawana visa ama vitambulisho halali, hali iliyoleta utatanishi mkubwa .

    Gazeti hilo limeeleza kuwa mwanadiplomasia wa Uganda ambaye hakutaka jina lake kutangazwa, amesema Waganda wengi wanaoishi Guangzhou bila vibali halali wanahofia watagunduliwa kuwa wanaishi isivyo halali kama wakienda kupimwa virusi. Mwanadiplomasia huyo pia amesema mwanzoni mwa mwaka huu, wakati mji wa Wuhan ulipoathiriwa vibaya na virusi vya Corona, serikali ya China ilizindua upimaji wa lazima kwa watu wote wa hali mbalimbali walioko maeneo hatarishi kwa maambukizi ya virusi vya Corona. Wakati huohuo, ubalozi mdogo wa Uganda mjini Guangzhou ulifanya maarifa ya kufanikiwa kuwapa msamaha Waganda wasiokuwa na vitambulisho halali. Lakini baada ya miezi miwili hivi, serikali ya China imeamua kumaliza maambukizi ya virusi hivyo kwa kina, na maafisa wa China wakaongeza bidii zaidi kukagua nyaraka za hali ya afya. Maelekezo yaliyotolewa na Ofisi ya Mambo ya Nje ya serikali ya mtaani mjini Guangzhou tarehe 5, mwezi huu yameelekeza kuwa wageni ambao hawakupimwa virusi vya Corona baada ya kuingia China wanatakiwa kufanyiwa vipimo hivyo bure kwa kuwasiliana na wafanyakazi wachina katika makazi yao. Wakishapimwa na kuonekana hawana virusi vya Corona, wanapewa QR Code. Watu wote wanahitaji kuonyesha picha ya QR ya afya wakati wanaingia sehemu za umma kama makazi, hoteli na maduka, na sera hiyo inatumika kwa wachina na wageni wote bila kujali utaifa. Maelekezo hayo yalizusha hofu miongoni mwa Waafrika wasiokuwa na vitambulisho halali, na pia Wachina wanaomiliki nyumba kwani wanajua wameenda kinyume na sheria kwa kupangisha vyumba kwa wahamiaji haramu. Kwa hivyo, ili wasigunduliwe na kukamatwa na polisi, wenye nyumba hao waliwataka wapangaji kuondoka kwenye nyumba zao na kujifanya kutokuwa na uhusiano na wapangaji hao. Ndio maana baadhi ya waafrika wamedai kuwa wenye nyumba wamewafukuza kwenye nyumba wanazoishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako