Utafiti umeonesha kuwa karibu asilimia 42 ya biashara nchini Afrika Kusini haziwezi kuendelea kutokana na zuio la taifa linalolenga kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.
Utafiti uliofanywa na idara ya takwimu ya Afrika Kusini, wafanyabiashara waliulizwa jinsi msukosuko wa sasa ulivyoathiri uendeshaji wa biashara zao katika wiki mbili zilizopita kutoka Machi 30 hadi Aprili 13.
Jumla ya kampuni 707 katika sekta rasmi zimejibu hojaji kwenye utafiti huo, huku zikieleza athari zinazoletwa na maambukizi ya virusi vya Corona dhidi ya thamani ya biashara, nguvukazi, mauzo na oda kutoka nje, manunuzi, bei na kiwango cha kudumisha biashara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |