• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: UEFA wakana kutakiwa kuahirisha mashindano kwa mwaka mmoja

    (GMT+08:00) 2020-04-23 08:51:52

    Chama cha soka Ulaya (UEFA) kimepinga madai kuwa kuna pendekezo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa linawataka waahirishe michuano yote ya kimataifa hadi mwishoni mwa mwaka 2021 kwa sababu ya corona. UEFA inaamini hiyo sio sahihi kwa maana hiyo mpira utakuwa hauchezeki. Awali UEFA ilikubali kuahirisha michuano ya Euro 2020 baada ya kushauriana na WHO. Msemaji wa UEFA alinukuliwa akisema si sahihi kwamba WHO wamependekeza mpira usichezwe hadi mwishoni mwa mwaka 2021. WHO ndio walioishauri kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC) kuahirisha michuano yake kwa mwaka mmoja iliyokuwa ifanyike Tokyo na walishauri pia kuahirishwa kwa Euro 2020 kwa mwaka mmoja hadi 2021 sababu ya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako