Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor, amepuuzilia mbali wanaotaka atoe sehemu ya mali yake ya Sh 4.8 bilioni kusaidia katika vita dhidi ya janga la corona nchini mwake. Adebayor, ambaye alipata umaarufu alipoichezea Arsenal nchini Uingereza kabla ya kuvalia jezi za timu kadhaa ikiwemo Manchester City, Real Madrid, na Tottenham Hotspur, kwa sasa anachezea timu ya Olimpia Asuncion nchini Paraguay kwa kandarasi itakayomalizika Desemba 31, 2020. Amenukuliwa na vyombo vya habari akisema hawezi kutoa hata ndururu kusaidia katika vita hivyo kwa sababu si yeye alileta virusi hivyo nchini Togo. Togo imeshuhudia visa 88 vya maambukizi ya virusi hivyo, huku watu sita wakipoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |