Mkutano wa 13 wa Bunge la Umma la China (NPC) utaanza kikao chake cha tatu cha mwaka tarehe 22 mwezi ujao.
Uamuzi huo umefikiwa leo katika kikao cha 17 cha Kamati Kuu ya Bunge hilo kilichofanyika kuanzia tarehe 26 mwezi huu.
Kikao cha 15 cha Kamati hiyo kilichokutana Desemba mwaka jana, kilifanya uamuzi wa kuahirisha mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China uliopangwa kufanyika Machi 5 na kutoa mapendekezo ya ajenda za kujadiliwa kwenye mkutano huo.
Kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, kikao cha 16 cha Bunge hilo kilichofanyika Februari 20 kilitoa uamuzi wa kuahirisha mkutano wa 13 wa Bunge la Umma la China ili kutekeleza maamuzi makubwa na utaratibu yaliyotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China inayoratibu njia za kukabiliana na mlipuko wa virusi na maendeleo ya jamii na uchumi.
Wakati huohuo, mkutano wa tatu wa mwaka wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) umependekezwa kufanyika Mei 21 hapa Beijing.
Mapendekezo hayo yametolewa katika mkutano uliofanyika hivi karibuni na kuongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Wang Yang.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |