Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli amesema kwamba anafikiria kuruhusu Ligi Kuu ya Tanzania Bara iendelee kwa sababu hajasikia mwanamichezo hata mmoja kuathiriwa na virusi vya corona. Akihutuba wananchi kupitia Televisheni leo Chato, Rais Magufuli amesema kwamba kwa sababu wanamichezo hawajaathiriwa na corona kuwazuia ni kutaka waugue. Machi 17, mwaka huu TFF ilisimamisha ligi zake zote ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote. Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28. Kwa ujumla CAF nayo ilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kufuatia mlipuko wa virusi vya corona hadi hapo itakapaoamuliwa vinginevyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |