• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwaka jana baraza la serikali la China lilishughulikia mapendekezo elfu 10  yaliyotolewa na wajumbe wa umma

    (GMT+08:00) 2020-05-10 19:51:23

    Msemaji wa baraza la serikali la China Bibi Xi Yanchun amesema, mwaka jana baraza hilo lilishughulikia mapendekezo 7,162 kutoka wajumbe wa Bunge la Umma na mapendekezo 3,281 kutoka wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa.

    Mwaka jana baraza hilo lilikubali mapendekezo zaidi ya elfu 3 na kutoa hatua elfu 1.5 za kisera, na nyaraka za kushugulikia mapendekezo hayo 6200 na kutoa habari 250 za kufahamisha. Kazi hizo zimesukuma mbele maendeleo ya mapambano dhidi ya kuondoa umaskini, kuongeza uwezo wa kuvumbua, kuimarisha mageuzi ya kuboresha huduma na kuunga mkono maendeleo ya makampuni madogomadogo.

    Bibi Xi pia amesema, wajumbe hao pia wametoa mapendekezo mazuri 400 katika kupambana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako