Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) imetoa ripoti ikisema, zuio kamili la mwezi mmoja kwa Afrika litagharimu asilimia 2.5 ya pato la jumla kwa mwaka barani humo, ambayo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 65.7.
Ripoti hiyo iitwayo COVID-19: Mikakati ya Uondoaji wa Karantini kwa Afrika, imesema zaidi ya nchi 42 za Afrika zimechukua hatua kiasi au hatua kamili za zuio ili kupambana na COVID-19. Ripoti imetoa mapendekezo mbalimbali kuhusu mikakati ya kuondoa zuio kwa nchi za Afrika, ikisema kufungwa kwa Afrika kunasaidia kupambana na virusi, lakini kutaathiri vibaya uchumi.
Kamati ya ECA pia imesema suala nyeti zaidi linalowakabili watunga sera ni athari ya kufungwa kwa Afrika kutokana na COVID-19 kwa usalama wa chakula.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |