Klabu za Ligi Kuu ya Uingereza zinatarajiwa kulipa jumla ya sawa na Sh za Kenya bilioni 47 kwa kampuni zitakazorusha mechi zao za kitaifa na kimataifa hata kama michuano tisa iliyosalia msimu huu itachezwa bila mashabiki. Timu zote 20 za EPL zilionywa kwamba huenda kiasi hicho cha fedha kikaongezeka zaidi iwapo msimu huu mzima utafutwa au kusiwepo na timu yoyote itakayoshushwa ngazi katika ligi ya msimu huu. Vinara wa klabu zote husika za EPL walikutana Mei 11, 2020 kuzungumzia uwezekano wa kurejeshwa kwa mechi 92 za msimu huu huku masuala kuhusu mipangilio ya kutoruhusu kikosi chochote kucheza katika uwanja wake wa nyumbani yakizingatiwa zaidi. Isitoshe, wasimamizi wa klabu zote husika za EPL wameombwa kufanikisha mipango ya kurejesha fedha za baadhi ya mashabiki waliokuwa wamelipia ada za kutazama mechi zote za vikosi vyao muhula huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |