• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya waweka juhudi mbalimbali kupambana na Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-14 09:07:18

    Wakati visa vya maambukizo vikiendelea kuongezeka nchini Kenya raia wa Kenya wanaonekana kuchukua tahadhari huku wengine wakiongeza juhudi za kibinafsi katika kukabiliana na virusi hivyo nchini Kenya.

    Ni saa mbili asubuhi katikati ya jiji la Nairobi na ninakutana na John Njenga ambaye anaendelea kupongezwa na wengi kutokana na juhudi zake za kuimarisha usafi ili kufanikisha juhudi za kukabiliana na maambukizo ya virusi vya Corona nchini Kenya. Njenga ambaye ni dereva wa matatu anasema anasema baada ya kusikia kilio cha waziri wa afya Bw Mutahi Kagwe alijinyima na kutumia akiba yake na kununua matangi matano ambayo amekuwa akiyajaza maji na kuyaweka katikati ya mji wa Nairobi ambapo watu wanaweza kunawa mikono kama mojawapo ya njia za kuimarisha usafi na hatimaye kuzuia maambukizo ya virusi vya Corona.

    Juhudi hizi za wakenya zinakuja wakati ambapo idadi ya maambukizo nchini Kenya imefikia 737 baada ya watu wengine 22 kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona hiyo jana. Hadi kufikia sasa serikali ya Kenya imepima jumla ya watu elfu 35432 na kuripoti vifo 40 kutokana na ugonjwa huo. Kenya pia imesema iliandaa shughuli ya kuwapima madereva wa Malori katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga ambapo zaidi ya madereva 20 kutoka Tanzania walipatikana kuwa na virusi hivyo. Kufuatia taarifa hiyo Wakenya wa kawaida nilioongea nao walionekana kuchukua tahadhari ambapo wengi wao wanasema hali inaonekana kuwa mbaya zaidi hivyo kuna haja ya kulinda familia zao.

    Baadhi ya kaunti ambazo zimeonekana kuwa na idadi kubwa ya maambukizo ni Nairobi na Mombasa. Kaunti ya kilifi ambayo idadi ya maambukizo ilikuwa juu imeonekana kufanya vyema baada ya kutoripotiwa visa vya maambukizo kwa karibu mwezi mmoja katika kaunti hiyo. Bw Amason Jeffah Kingi ni Gavana wa kaunti hiyo ya Kilifi. Anasema kama kiongozi ilimlazima kuonyesha mfano mwema kwa kujiweka chini ya karantini kitendo ambacho kilichochea wenyeji wengi kuchukua hatua.

    Hadi kufikia jana jumla ya watu 281 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya watu wengine 22 kupona ugonjwa huo hapo jana. Wachambuzi wa mambo ya afya wanaona hatua mbazo Kenya imechukua zinaonekana kuzaa matunda na wakenya wengi wanachukulia ugonjwa huo kuwa hatari. Hivi sasa tunasubiri kuona kama maagizo mapya ya serikali ya kukabiliana na janga hili yataendelea kuzaa matunda au la.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako